Idara ya Wanawake

 

IDARA YA WANAWAKEwamama

 

 1. Utangulizi

Idara ya wanawake ilianzishwa rasmi mwaka 1966. Maono ya idara ya wanawake ni kuwa chombo cha kuwawezesha wanawake/ wasichana, kushiriki kikamilifu katika mfumo mzima wa maisha katika masuala ya kiimani, kiuchumi na kijamii.

Lengo

Kuwa chumvi ikoleayo katika kuwezesha jamii, hususani wanawake kutambua nafasi (fursa) ya usawa, inayothibitika kwa misingi ya neno la Mungu kati ya wanawake na wanaume na kuheshimu misingi ya uumbaji na ukombozi bila ya ubaguzi wa kijinsia, kwa lengo la kujengwa kiroho, kiakili na kimwili.

 

 1. Lengo hilo hutimilika kwa:

 

 • Kuhimiza elimu ya imani kwa jamii hususani kwa wanawake, ili watambue na kuchukua nafasi inayowapasa katika jamii na kutumia vipawa vyao kikamilifu na bila hofu.
 •  Kuwezesha jamii hasa wanawake, kutambua kazi zao ili kuleta mahusiano ya amani katika familia.
 • Kulea vijana hususani wasichana katika hali inayowezesha kukua na kuishi katika maadili mema.
 • Kuinua kiwango cha ufahamu na ujuzi kwa wanawake ili kupata uwezo wa kushiriki katika masuala ya jamii na hata kuinua hali yao ya kiuchumi.
 • Kuendeleza na kuimarisha kazi za uinjilisti na mission ndani na nje ya dayosisi.
 • Kukuza mtandao wa utendaji kwa kushirikiana na asasi nyingine.

 

Idara pia inahusika na:

 

 • Kuandaa na kutuma Maombi ya Dunia kwa watu wazima na watoto sharikani na kwenye vituo kila mwaka mwezi wa tatu.
 • Kuandaa na kutuma kazi za kila mwaka sharikani.
 • Kuandaa maonyesho ya kazi za idara mara moja kila mwaka kwa kila jimbo.
 • Kuendesha mkutano mkuu wa idara kidayosisi, mara moja kila baada ya miaka miwli, ambapo mada mbali mabali na mpango kazi wa kipindi cha miaka miwili huwekwa.
 • Kuandaa semina mbali mbali na mafunzo kama ya uongozi, ujasiriamali, haki za binadamu, utunzaji wa mazingira, ustawi wa kiroho kwa makundi kama wanawake, wajane, Parish workers, wasichana n.k
 • Ziara mbalimbali za mafunzo
 • Kuandaa miradi ya kuinua kipato

 

Idara inakituo kiitwacho Angaza Women Centre chenye ekari 61, kinatoa mafunzo kwa wanawake.  Mpango kwa sasa ni kujenga Hosteli.

 

Mkuu wa Idara Mch.        Faustine Kawa M.

 

Leave a Reply