Idara ya Afya

Idara hii inasimamiwa na Bw.Julius Mwanga, ni idara iliyopo Makao Makuu ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini.  Idara hii inaratibu na kusimamia maswala ya afya ikiwa ni pamoja na matibabu kwa Hospitali zilizoko chini ya Dayosisi ya Kaskazini ambazo ni; Machame Council Designated Hospital, Marangu Lutheran Hospit na Karatu Council Designated Hospital.

Pia idara hii inaratibu na kusimamia mafunzo ya Uganga na Uuguzi yanayotolewa na  Vyuo vya Afya vilivyo chini ya Dayosisi ya Kaskazini ambavyo ni; Chuo cha Uganga na Uuguzi Machame na Chuo cha Uganga na Uuguzi Karatu.

Kitengo hiki kinatoa Huduma ya Elimu ya Afya kwenye Sharika, kusaidia miradi kama uchimbaji visima na Uvunaji wa  maji ya mvua na huduma nyingine.

Leave a Reply