UWAKILI NA UCHUMI

MCH. Andrew SUtangulizi:

Idara ya Uwakili KKKT Dayosisi ya Kaskazini inaongozwa na Mchungaji Andrew S. Munisi tangu Sept 2012 hadi sasa. Idara hii miaka ya nyuma iliongozwa na Marehemu Mchungaji Godwin Moshi ambaye aliitwa mbinguni May 1999. Baada ya hapo Idara iliongozwa na Mchungaji Godson Mosha hadi Sept 2012.

Wajibu wa Idara

Idara ya Uwakili na Uchumi  inawajibu wa kusisitiza  na kuelimisha washarika kutambua wito wao na  kuwafahamisha kuwa  Mungu ni Wakili wa kwanza ambaye aliweka vitu katika utaratibu na mpango mzuri wa kumwezesha mwanadamu kuishi katika dunia hii (oder of creation). Kanisa lina wajibu mkubwa sana wa kupokea kwa shukrani, kutunza, kutumia mali tulizopewa na Mungu kwa neema hasa kwa  kutoa hesabu ya vyote walivyopokea kwa mwenye Mali ambaye ni Mungu mwenyewe.

Idara ya Uwakili inawajibika kuwakumbusha wachungaji na washarika kuwa, Mkristo ni kiungo muhimu sana cha Kanisa. Kwa kuwa utajiri wa Kanisa ni washarika, ni muhimu sana kila kiongozi wa usharika na msharika ajitambue kuwa kiungo cha Mwili wa Kristo.  Kwa ubatizo tumefanywa kuwa mwili mmoja yaani Kanisa na Kristo ndiye kichwa cha mwili huo. Tu viungo vingi  muhimu vya mwili mmoja.  IKor. 12:12-30.

Idara hushauri viongozi wa sharika zote 164 na majimbo yake yote kwa kuelimisha washarika wake kuwajibika na kuwa na kipato halali ikiwa ni kwa njia ya ufugaji, kilimo, Biashara na kazi za kuajiriwa  n.k, ili waweze kutoa sadaka iliyoandaliwa vvema ikiwa  ni wajibu na heshima kwa Mungu.

Idara pia inahusika katika kuandaa na kuwasilisha ratiba na miongozo kuhusu somo la Uwakili pote katika Sharika zake.

Idara hufuatilia kwa karibu sana kwa ushirikiano na  Hazina Kuu  ya Dayosisi matoleo yote ya sadaka zote ndani ya sharika na kuona usahihi wa utoaji na utunzaji wake.

Idara inaratibu uandaaji na usambazaji wa vifaa vya matoleo ikiwa ni bahasha za ahadi, vitabu vya kumbukumbu za ndoa, ubatizo, mazishi, Kipaimara, n.k

Idara inaratibu  uandaaji wa semina  za mafundisho ya  uwakili na maongozi ya sharika  kwa  viongozi wa ngazi zote za  sharika.

Pia idara huandaa na kutafsiri takwimu za washarika wanaohudumiwa na dayosisi ya Kaskazini, ikiwa ni pamoja na uratibishaji wa Mikutano Mikuu ya Dayosisi kwa kushirikiana na Idara ya Mawasiliano.

“Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; mtumikieni BWANA kwa furaha; njooni mbele zake kwa kuimba; jueni kwamba BWANA ndiye Mungu.”

Mch. Andrew S. Munisi

IDARA YA UWAKILI NA UCHUMI

Simu No: +255754844511