Elimu ya Kikiristo

IDARA YA ELIMU YA KIKRISTO

1.     UTANGULIZIelimu ya kkristo

Idara  ina madawati matatu

 • Dawati linalohusika  na watoto hasa wa Shule za Montessori na Sunday School
 • Dawati linalohusika na dini Shuleni, Kipaimara na malezi ya washarika kwa jumla
 • Dawati linalohusika na mashule hasa shule za Sekondari na Vyuo
 1. 2.     MADHUMUNI YA IDARA
 • Kuratibu huduma yote ya malezi ya Kiroho kwa washarika na marika yote.
 • Kuratibu shughuli zote za mafundisho ya Sunday School na dini Shuleni
 • Kuratibu shughuli zote za kupata nyenzo za kufundishia na kujifunza kwa watu wa marika yote.
 • Kuratibu shughuli zote za kupata wafundishaji na kuwajengea uwezo wa kufundisha.
 • Kukagua na kupima uendelezaji wa malengo ya idara
 1. 3.     VITENGO VYA IDARA NA KAZI ZAKE

3.1.                     Kitengo cha Shule za montesori

 • Kuhimiza kila usharika kuwa na Shule za montesori
 • Kushirikiana na chuo cha montesori cha Ushirika wa Neema kuona kuwa waalimu wanaandaliwa vizuri wanapokuwa  kozi, wanakaguliwa na wanafunzika vizuri
 • Kuhakikisha Shule za montesori za Sharika ni za viwango stahiki na zimeandikishwa kisheria
 • Kuhakikisha waalimu wa montesori Sharikani na Vituoni wanatunzwa vizuri, na kuongezewa uwezo wa utendaji
 • Kuhimiza kuwepo shule za kutosha na ziwe karibu na watoto; ili waweze kwenda kila siku na kurudi nyumbani

3.2.                     Kitengo cha Shule za Juma pili kwa watoto( Sunday School)

 • Kusimamia mtaala wa kufundisha shule hizi
 • Kuwajengea waalimu uwezo wa kufundisha
 • Kusimamia upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia na kufundishia
 • Kuhimiza uwepo wa waalimu wa kutosha
 • Kuhimiza kuwepo kwa madarasa ya kutosha
 • Kuandaa sikukuu ya Mikaeli na watoto kidayosisi

3.3.                     Kitengo cha Kipaimara

 • Kuratibu uandikishaji wa wanafunzi wa kipaimara
 • Kuandaa na kusambaza nyenzo za kujifunzia na kufundishia
 • Kuwajengea waalimu uwezo wa ufundishaji
 • Kukagua ufundishaji
 • Kutathimini uelewa wa wanafunzi

3.4.                     Kitengo cha Dini Shuleni

 • Kuhakikisha nyenzo za kujifunzia  zinapatikana
 • Kuhakikisha waalimu wakutosha wapo
 • Kuhakikisha madarasa yakutosha yapo
 • Kuwatia moyo wafundishaji na kuwajengea uwezo
 • Kukagua ufundishaji
 • Kupima ufanisi wa kazi

 

3.5.                     Kitengo cha Ibada  za katikati ya Juma

 • Kuratibu ibada hizi kidayosisi
 • Kuratibu uandaaji wa masomo na usambazaji wake
 • Kutathimini mwenendo mzima wa Ibada hizi

3.6.                     Kitengo cha bible study na Fellowship

 • Kuratibu masomo yanayofundishwa
 • Kuwajengea uwezo wasimamizi na wafundishaji

3.7.                     Kitengo cha Uinjilisti

 • Kushirikiana na idara ya misioni na uinjilisti, katika kuratibu mikutano ya Injili
 • Kuandaa mahubiri na mikutano ya injili
 • Kuhimiza Uinjilisti

3.8.                     Kitengo cha maombi

 • Kuratibu maombi
 • Kuhimiz maombi sharikani na hasa kwa viongozi sharikani
 • Kuratibu maombi na maendeleo mengine

3.9.                     Kitengo cha maandiko

 • Kuhakikisha maandiko yote yanayohitajika kwa malezi ya kiroho yanapatikana na kuwafikia  walengwa.
 • Kuandaa maandiko kwa njia ya warsha na kuyasambaza
 • Kuwasiliana na watoaji wa vitabu vya malezi ili kuona wanatoa maandiko yenye ubora na viwango stahiki.

 

 

 

 

 

/p