Umoja Hostel

Umoja Lutheran Hostel

Umoja Lutheran Hostel ni Kituo Kilicho chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini.   Kituo hiki mwanzoni kilijulikana kama Women Hostel,  kikitoa huduma kwa Wamama waliokuwa wanapata shida ya usafiri usiku pamoja na Mabinti walioajiriwa Moshi kabla hawajapata Nyumba za kuishi.

Umoja Lutheran Hostel kwa sasa inatoa huduma za Kumbi za Mikutano, Chakula, Vyumba  vya  kulala na huduma nyingine nyingi.