Faraja Primary

faraja

Shule ya Msingi Faraja (Maalumu kwa Watoto wenye Ulemavu wa Viungo) inamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini.  Shule hii ilijengwa ili kuwawezesha watoto wenye ulemavu wa viungo, wenye uwezo wa kukaa darasani na kupokea vizuri masomo waweze kupata nafasi ya kupata Elimu. Shule ipo Wilaya ya siha, km 10 kutoka mji mdogo wa Sanya Juu.

faraja2

 

 

Shule ilianza kujengwa mwaka 2000 na KKKT Dayosisi ya Kaskazini ikishirikiana na Bw. Donald Tolmie na Mkewe Joan wa Norfolk Virginia U.S.A.  Shule ilifunguliwa rasmi 2001, Julai.  Shule ni ya Bweni  kwa Wasichana na Wavulana.