Jimbo La Kilimanjaro Mashariki

masharikiKijeografia, Jimbo la  Kilimanjaro Mashariki kabla ya mwaka 1982, lilienea katika        wilaya mbili kiserikali; Wilaya ya Moshi vijijini na Wilaya ya Rombo, zikiwepo pia sharika za manispaa ya Moshi.

Mwaka 1982 Jimbo liligawanywa na kutokea jipya la Kilimanjaro Kati. Jimbo la Kilimanjaro Mashariki  kwa sasa linaanzia Kirua hadi Kamwanga Wilaya ya Rombo.

Jimbo lina jumla ya sharika 44 kwa sasa na mwaka 2014 utazaliwa Usharika mpya wa Nganyeni. Utakaogawanyika kutoka Usharika wa  Msae, ambao utafanya sharika ziwe 45.  Jimbo lina jumla ya washarika  122,666; ambapo watu wazima ni 85,127 na watoto ni 37539.

Viongozi walioongoza Jimbo

Mkuu wa Jimbo wa kwanza alikuwa Mch. Benjamen Moshi (1945- 1960), Mch. Kalebi Mangesho(1960-1972), Mch. Martin F. Shao (1973-1976), Mch. Elisante J. Mamuya (1976-1988), Mch.Luka M. Kessi (1989-2011) na Mch. Winford J. Mosha (2012 hadi sasa).