Jimbo La Kilimanjaro Kati

Jimbo la Kilimanjaro Kati lilianza mwaka 1982, January; likiwa na jumla ya sharika 12 zilizokuwa zimeanzishwa katika stesheni ya Moshi. Sharika hizo ambazo ni Kidia, Mbokomu, Tella, Mowo, Shia, Sango, Kahe, Moshi Mjini, Moshi Kati, Arusha Chini na Chemchem, zilikuwa sehemu ya Jimbo la Kilimanjaro Masharika kabla ya Kuanza Jimbo la K/ Kati.

Jimbo la Kilimanjaro Kati hadi sasa lina jumla ya Sharika 34 ambazo ni Chekereni, Foyeni, Fukeni, Karanga, Kiboriloni, Kidia, Kikarara, Kisamo, Kiwalaa, Kiyungi, Kyomu, Longuo, Lowasi, Lowiri, Lyamanyaki, Maedeni, Magadini, Mahoma, Majengo, Mande, Mdawi, Moshi Mjini, Moshi Pasua, Mowaleni Komfuru, Mowo, Msaranga Mandaka, Msitu wa Tembo, Mwangaria, Natiro, Rau, Shia, TPC, Tella na Uru.

Jimbo hili lina Jumla ya Washarika 73,218 wakiwamo watu wazima 29,840 na watoto 43,378.

Kijeografia, Jimbo la Kilimanjaro Kati limeanzia Kibosho hadi mto Nanga kufuata barabara iendayo Dar es salam upande wa kulia hadi unapoingia Mwanga Upareni.

Jamii ya Jimbo la Kilimanjaro Kati wanajishughulisha na Kilimo, Ufugaji pamoja na Biashara.

Jimbo limewahi kuongozwa na Mkuu wa Jimbo Mch. Joseph Ringo ambaye ndiye aliyekuwa Mkuu wa jimbo wa Kwanza wa Jimbo la Kilimanjaro Kati, akafatiwa na Mch. Elingaya Saria ambaye ndiye Mkuu wa Jimbo hili hadi sasa