Jimbo la Karatu

Mkuu wa Jimbo la Karatu
Mkuu wa Jimbo la Karatu

Jimbo la karatu (Mbulu Hanang) lilitokana na Jimbo la Maasai mbulu. kabla ya mwaka 1971 Jimbo la Maasai Mbulu lilikuwa jimbo mojawapo ya majimbo 6 ya Dayosisi ya Kaskazini  ambayo ni:

 1. Jimbo la Pare
 2. Jimbo la Kilimanjaro Mashariki (Jimbo la Kilimanjaro Kati halikuwepo)
 3. Jimbo la Kilimanjaro Magharibi(Jimbo la Siha halikuwepo)
 4. Jimbo la Meru
 5. Jimbo la Arusha na
 6. Jimbo la Maasai Mbulu

Miaka ya 1971 eneo la Babati-Magugu, Kilimamoja na Oldeani- Mang’ola iliomba kuwa jimbo toka jimbo la Maasai Mbulu kwa sababu ya upana wa maeneo ya kazi na Halmashauri Kuu ya Dayosisi ilipokea ombi hilo, jimbo la Mbulu Hanang likaundwa kutoka katika jimbo la Maasai Mbulu.

Mkutano wa kwanza wa jimbo la Mbulu Hanang, uliandaliwa  kukutana Oldeani  tarehe 27-28 Septemba  1972. Mkutano huo uliwachagua  viongozi wa Jimbo la Mbulu Hanang. Mkuu wa jimbo  Mch. Gabriel. Q. Bayda na Mkuu wa pili wa jimbo Mch. Bumija Mshana walichaguliwa   .

Mkutano huo ulithibitisha makao makuu ya jimbo  la Mbulu- Hanang kuwa Makuyuni. Ofisi ya muda ilianzishwa pale Karatu Station mwaka 1972 -1989.

Januari 1, 1973, eneo la Sonjo ilijiondoa nakuwa Sinodi ya mkoani Arusha, kwasababu hiyo  Mch. Bumija Mshana akajiunga na Sinodi ya Mkoani Arusha akitokea jimbo la Mbulu Hanang.

Jimbo la Mbulu Hanang likabaki na Sharika mbili; Karatu- Kilimamoja na Oldeani –Mang’ola wakiwa na wachungaji wawili; Mch. Gabriel. Q. Bayda na Mch. Joseph Bee.

krt4Jimbo la Karatu (Mbulu Hanang) kwa sasa lina jumla ya Sharika 12 ambazo ni:

 1. Usharika wa Mang’ola
 2. Uaharika wa Baray
 3. Usharika wa Oldeani
 4. Usharika wa Qurus/ Endashang’wet
 5. Usharika wa Bashay
 6. Usharika wa Karatu Mjini
 7. Usharika wa Basodawish
 8. Usharika wa Endamarariek
 9. Usharika wa Endallah
 10. Usharika wa Rhotia
 11. Usharika wa Karatu Mjini
 12. Usharika wa Kilimamoja

Jimbo la Karatu lina jumala ya washarika 43454, ambapo wanaume wako 26,727, wanawake 5,493 na watoto 17,774 kwa sharika zote 12. Sharika hizi kumi na mbili zina mitaa Hamsini na tisa.

Dayosisi ina vituo vitatu kwenye jimbo lake la Karatu ambavyo ni:

 1. Karatu Lutheran Hospital DDH-Hospitali teule ya Wilaya ya Karatu
 2. Karatu Lutheran VTC- Chuo cha Ufundi Lutheran Senta
 3. Karatu Lutheran Hostel
Mazingira ya Karatu Hospital
Mazingira ya Karatu Hospital
Mazingira ya karatu VTC
Mazingira ya karatu VTC
Mazingira ya Karatu Hotel
Mazingira ya Karatu Hotel

 Pia kuna duka la vitabu na vifaa vya stationary- Christian Bookshop pamoja na shamba la ekari 150 ambalo mpango ni kupanda miti, lakini kwasasa Jimbo lina wakodisha kwa wakulima wa Mahindi na Ngano.

Jimbo la Karatu limeongozwa na wakuu wa majimbo 5 hadi sasa. Mkuu wa kwanza wa jimbo alikuwa Mch.Gabriel. Q. Bayda (1972-1983), akafatiwa na Mch. Baha (1983-1987), Mch Gabriel Bayda aliongoza jimbo kipindi cha awamu ya tatu tena(1988-2008). Awamu ya nne aliongoza  Mch. Natse (2008-2010). Baada ya Mch. Natse alichaguliwa Mch. Samweli Silaha kuwa mkuu wa jimbo kuanzia October 2010 hadi sasa.