Jimbo la Hai

hai

Jimbo la Hai ni moja kati ya Majimbo matano (5) ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini.    Jimbo hili lipo katika eneo la Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro kwa sehemu kubwa na Sehemu limeingia katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara (Usharika wa Nomeuti)   na Wilaya ya Moshi Vijijini (Usharika wa Kikavu Chini).
Makao Makuu ya Jimbo la Hai yapo Bomang’ombe Kwenye Makutano ya Barabara ya Kwenda Westi Kilimanjaro Km 20 toka Moshi Mjini.
Jimbo lina Jumla ya Sharika 48 na Mitaa 100.  Idadi ya Washarika wote ni 90,782 ambapo Wanaume wapo 21,753, Wanawake 30,146 na Watoto wapo 38,883

Jimbo limegawanyika katika kanda Tano ambazo ni:
Machame Mashariki
Machame Mangaribi
Masama Mashariki
Masama Magharibi na
Kusini.