Jimbo la Siha

Jimbo la Siha lilianza kwa kugawanyika toka lililokuwa Jimbo la Kilimanjaro Magharibi mwaka 1987 likaitwa jimbo la Hai Magharibi na Mkuu wa Jimbo wa kwanza alikuwa Mch. Eligard V. Nassari.

Jimbo hili lilianza likiwa na jumla ya sharika kumi na moja (11).  Sharika hizo zilikuwa; Siha Livishi, Ivaeny, Fuka, Sanya Juu, Wiri, Ngaritati, Kyengeru, Kashashi, Olmolog, Engarinairobi na Kyungukyelwa.

Kufikia sasa Jimbo lina jumla ya Sharika 21, mitaa 71, Wakristo Walutheri watu wazima 15,924 na Watoto 17,544 kwa takwimu za mwaka 2010.

Jimbo la Hai Magharibi lilibadilishwa jina lake nakuitwa Jimbo la Siha mwaka 2006, mara baada ya eneo la Siha kuwa Wilaya Kamili nakuitwa jina la Siha.