Karatu VTC

Karatu Lutheran VTC inamilikiwa na KKKT Dayosisi ya Kaskazin. Chuo hiki kipo kwenye jimbo la Karatu; Jimbo la Karatu ni mojawapo kati ya majimbo 5 ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini.

Karatu VTC
Karatu VTC

Chuo cha Karatu Lutheran VTC kilianzishwa mwaka 1998. Kilianza kama chuo cha Sayansi Kimu (Ushonaji na Upishi).  Mwaka 2000 chuo kilianzisha Programu ya Useremala na kufanya kuwepo na fani 2 (Sayansi Kimu na Useremala). Kufikia mwaka 2002 fani zilitenganishwa kukawa na fani 3, ambazo ni:

  1. Upishi
  2. Ushonaji na
  3. Useremala

Mwaka 2009 chuo kilisitisha fani ya useremala kutokana na kutokuwepo kwa wanafunzi waliojiunga kwa fani hiyo (Wengi wao walijifunza fani hii huko mitaani hivyo chuo hakikupata wanafunzi na kuamua kusitisha fani hiyo ya useremala) na badala yake kukaanzishwa fani ya Umeme Mwezi Machi 2012.

LIcha ya kuwepo kwa fani hizi tatu ( Fani ya Umeme, Fani ya Upishi[Hotel Management], na Fani ya Umeme), chuo kina masomo bebezi ambayo ni:

  1. Somo la Kiingereza
  2. Somo la Ujasiriamali
  3. Somo la Kompyuta
  4. Somo la Hisabati
  5. Somo la Dini na Malezi

Masomo haya hutolewa kwa wanafunzi wa fani zote tatu.

Wanafunzi wakiwa katika Somo la Computa
Wanafunzi wakiwa katika Somo la Computa
Mazingira ya Chuo cha Karatu VTC
Mazingira ya Chuo cha Karatu VTC

Chuo kimesajiliwa na Veta mwaka 1998 na kina jumla ya wanafunzi 59 hadi sasa.

 

Jesca Lazaro - Mkuu wa Chuo cha Karatu Luth. VTC
Jesca Lazaro – Mkuu wa Chuo cha Karatu Luth. VTC

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkuu wa Chuo: Mwalimu Jesca Lazaro

Mobile No. +255 (0) 767851066

Email: karatuvtc2013@gmail.com

karatuvtc@northerndiocese.co.tz