Shule ya watoto ya jumapili (sunday School)

Sunday School ni ibada maalumu kwa watoto. Ibada hizi zinaendeshwa kwa mfumo wa mafunzo maalumu yanayolenga kumjenga mtoto mdogo katika Kumjua mungu, na zaidi kumjengea msingi imara wakati wa ukuaji wake akue kimwili na kiroho na kuwa raia mwema na mwenye mafanikio yote kimwili na kiroho. Huduma hii muhimu inaratibiwa na dayosisi kupitia idara ya elimu ya kikristo. katika kutimiza majukumu yake idara inafanya mambo yafuatayo:

  • Kusimamia mtaala wa kufundisha shule hizi
  • Kuwajengea waalimu uwezo wa kufundisha
  • Kusimamia upatikanaji wa nyenzo za kujifunzia na kufundishiasunday
  • Kuhimiza uwepo wa waalimu wa kutosha
  • Kuhimiza kuwepo kwa madarasa ya kutosha

 

Leave a Reply