Wiki ya Injili

Oktoba 31, 2018, Mhe.  Mkuu wa KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo alizindua rasmi wiki ya Nuru ya Injili ambapo mwaka huu imefanyika katika Jimbo la Hai. Wahubiri 244 pamoja na kwaya za matarumbeta walifanya maandamano katika maeneo mbalimbali ya mji wa Boma kisha kupokelewa na Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo pamoja na Mhe. Msaidizi wa Askofu Mch. Elingaya Saria kisha kuelekea katika sharika zote 49 za jimbo la Hai kuhubiri Injili.
Katika salam za Mhe. Baba Askofu Dkt. Shoo, alisistiza katika kulisikia neno la Mungu na Kulitii.