Kilele cha Jubilii ya Miaka 125

ya Injili tangu wamisionari wa kwanza kutoka chama cha misioni cha Lepzig Nchini Ujerumani walipowasili Nkwarungo mwaka 1893 kilifanyika katika  Usharika wa  Nkwarungo Machame Oktoba 21, 2018.   Dayosisi sita za KKKT ambazo kwa pamoja zilisherehekea jubilii hii
ni pamoja na Dayosisi ya Kaskazini,  Dayosisi ya Kati, Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dayosisi ya Mwanga,  Dayosisi ya Pare na Dayosisi ya Meru.