Mikaeli na Watoto

Ni kwenye sikukuu ya Mikaeli na watoto Septemba 30, 2018 Mhe Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo, Msaidizi wa Askofu Mch.Elingaya Saria, Katibu wa Idara ya Elimu ya Kikristo Mch. Rickenson Moshi wakiwahudumia watoto keki waliyoandaliwa kwenye sherehe yao.

Kidayosisi sikukuu ya Mikaeli na watoto
2018, imefanyika katika Usharika wa Kotela Jimbo la K/Mashariki.

Katika hadhira hiyo, Mhe. Baba Askofu Dr Fredrick Shoo aliwapongeza na kuwashukuru walimu wa shule ya Jumapili kwa kazi nzuri wanayofanya.

Kadhalika aliwaasa watoto kuwa watii  kwa wazazi wao katika mema pekee  na kamwe kutokukubali  kushawishiwa kufanya dhambi kwa  kigezo cha kutii.

Naye  Msaidizi wa Askofu Mch Elingaya  Saria aliwataka  wazazi kuacha kuwakosesha watoto kwa namna yeyote na badala yake waongeze juhudi  katika malezi hasa wakati huu ambao dunia imeharibika.