Sikukuu ya Uimbaji DK 2018

Sikukuu ta Uimbaji  na vijana katika Dayosisi ya Kaskazini ilifanyika Oktoba 7,2018. Jumla ya kwaya 18 zilishiriki katika uimbaji huo.
Wenyeji wa Uimbaji huo walikuwa Usharika wa Sanya Juu Jimbo la Siha.

Uongozi wa Dayosisi ulitoa pongezi kwa waimbaji wote, sharika zao na  Waalimu  kwa kazi nzuri ya kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo.

Katika uimbaji huo shule ya sekondari Natiro  ilishika nafasi ya kwanza katika kwaya za Sekondari Mchanganyiko na Sekondari ya Masama  ilishika nafasi ya kwanza katika Sekondari za Wasichana.

Kwa upande wa kwaya za vijana kwaya ya Kingereka ilishika  nafasi ya kwanza
na Shiri kushika nafasi ya kwanza katika kwaya za Mchanganyiko Sharikani.

Kwa kwaya za tarumbeta kwaya ya  Moshi Mjini ilishika nafasi ya kwanza

Kwaya zote zilipokea matokeo kwa furaha na  kwaya zilizoshiriki zilikabidhiwa Cheti Cha ushiriki pamoja na zawadi nyingine.