Mahafali Mwika Bible College

Chuo cha Kilutheri cha Biblia na Theologia Mwika kimefanya Mahafali ya 65 ya kuhitimisha wanafunzi 85 kwa kozi mbalimbali Jumapili ya Oktoba 14, 2018.

Mkuu wa KKKT, Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliwatunuku vyeti wahitimu hao 85 ambapo kati yao 15 wamehitimu kozi ya Msingi Elimu ya Kikristo na Uinjilisti ngazi ya cheti, wanafunzi 13 kozi ya Muziki ngazi ya cheti, Wanafunzi 15 kozi ya Juu Elimu ya Kikristo na Uinjilisti ngazi ya cheti,  Wanafunzi 8 kozi ya Wasaidizi wa Sharika, huduma za jamii na wanafunzi na 34 wamehitimu Theologia ngazi ya cheti.