Sharika 10 zapokea tuzo ya Moyo wa Kijani

Mkuu wa KKKT ambaye pia ni Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Mhe. Baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo ametoa tuzo ya Moyo wa kijani kwa sharika 10  kati ya sharika 40 zilizofanya vizuri katika huduma ya udiakonia kupitia mpango wa UYAMWI wa kuhudumia makundi ya watu wenye uhitaji maalumu.

Sharikika hizo 10 ziliongozwa na usharika wa Hai Mjini uliofanya vizuri zaidi miongoni mwa sharika 40 zilizojiunga na mpango wa UYAMWI tangu kuanzishwa kwake mika 14 iliyopita.

Akikabidhi tuzo hizo Mkuu wa KKKT alitoa wito kwa sharika zote za Dayosisi ya Dayosisi kuanzisha  kamati za diakonia kupitia UYAMWI kwa lengo la kutoa huduma kwa makundi ya watu wenye uhitaji maalumu.