Welcome To ELCT Northern Diocese

Mkuu wa KKKT na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini

K.K.K.T  Dayosisi ya Kaskazini (ambayo ilijulikana kama “Kanisa la Kilutheri la Tanganyika ya Kaskazini kabla ya mwaka 1963)  lina makao yake makuu Mjini Moshi kilimanjaro mkabala na stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani.

K.K.K.T Dayosisi ya Kaskazini ina majimbo matano: Karatu, Siha, Hai, Kilimanjaro Kati na Kilimanjaro Mashariki. Dayosisi ya Kaskazini imahusika kwa karibu katika uanzishwaji Dayosisi ya Kati, Kaskazini Kati, Meru na Pare. Kwa sasa inalea Dayosisi ya ziwa Tanganyika iliyokuwa ikijulikana kama Misioni ya Rukwa kabla ya mwaka 2014. Kwenye umoja na Dayosisi nyingine za K.K.K.T, imehusika kuanzisha na/ au kulea makanisa ya Kilutheri Congo DRC, Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Uganda na Zambia.

Taswira (Vision) :

Kuwa kanisa linaloongozwa na Roho Mtakatifu, lililojaa waamini wenye afya nzuri,wenye elimu nzuri, waliofurika furaha, upendo na amani; waliobarikiwa kimwili na kiroho na watakao urithi uzima wa milele katika Yesu Kristo.

Dhamira (Mission) :

Kuwawezesha watu wote wamwamini na kumtegemea Mungu katika yesu Kristo ili wawe na uzima tele kwa kuwafundisha habarinjema zinazopatikana katika Neno la Mungu kama ilivyo katika Biblia na mafundisho ya kanisa la kilutheri ili waurithi uzima wa milele.

Kwa kufanya hivyo K.K.K.T – D.K inalenga kujenga kanisa na jamii ya watu wanaojitegemea, wanaojali na kutafuta amani, upendo, usafi wa roho na maendeleo ya pamoja na ya binafsi.

Askofu Mstaafu Dr. Martin F. Shao
Askofu Dr. Martin F. Shao Askofu wa Tatu, Dayosisi ya Kaskazini
kweka
Askofu Dr. Erasto N. Kweka Askofu wa pili, Dayosisi ya Kaskazini
Marahemu. Askofu Stefano Moshi. Askofu wa kwanza wa Dayosisi ya Kaskazini
Marahemu. Askofu Stefano Moshi.
Askofu wa kwanza wa Dayosisi ya Kaskazini